Katika makala ambayo aliisoma bwana Robert Kiyosaki anatuambia kuwa ilikuwa inaonesha kwamba asilimia 70 ya kipato cha matajiri kinatokana na vyanzo mbalimbali walivyowekeza na asilimia chini ya 30 ndio inayotoka kwenye mshahara, na kama waliajiriwa basi ni wafanyakazi katika kampuni zao.
Kwa watu wengine, maskini na watu wa daraja la kati... karibia asilimia 80 ya kipato chao kinatokana na mshahara (kuajiriwa au kujiajiri) na chini ya asilimia 20 kutoka kwenye vyanzo walivyowekeza. (HAPA NI CHANGAMOTO KWETU KAMA TUNATAKA KUWA MATAJIRI SIKU MOJA…INATUPASA TUPAMBANE TUFIKIE WALAU ASILIMIA 70 KUTOKA KWENYE UWEKEZAJI WETU)-------MUNGU ATUJALIE
NINI MAANA YA UTAJIRI?
Wengi wetu tunafahamu kuwa TAJIRI ni mtu mwenye pesa nyingi au mtu anayetengeneza pesa nyingi kwa mwezi. Ila UTAJIRI hautazamwi kwa kuangalia kiasi cha pesa unachozalisha kwa mwezi au kiwango cha pesa ulicho nacho….UTAJIRI unaangaliwa kwa idadi ya siku ambazo utaweza kuishi bila ya wewe au mtu yeyote katika familia yako kufanya kazi. Kwa mfano, matumizi yako au ya familia yako ni laki 2 (200,000/=) kwa mwezi na wewe katika akiba yako una sh. Milioni moja (1,000,000/=) manake UTAJIRI wako ni wa miezi mitano (5) au siku 150 tu.
Kinachotakiwa ni kuhakikisha kuwa tunawekeza mpaka kufikia mahali ambapo vipato vyetu kwa mwezi vinazidi matumizi yetu. Kwenye suala la UTAJIRI shida sio kiasi gani cha pesa unachokizalisha kwa mwezi.....bali ni kiasi gani ambacho utaendelea kuwa nacho na kwa muda gani pesa hiyo itaendelea kukutumikia.
Watu wengi leo inawezekana wanatengeneza pesa nyingi lakini yote inaishia kwenye matumizi na kila muda wanapozalisha zaidi wanazidisha tena matumizi.
Kumbuka....Moja ya matatizo makubwa yanayotukumba watu wengi siku hizi ni mawazo (STRESS) yanayotokana na kufanya kazi kwa bidi lakini bado vipato havikidhi mahitaji (MATUMIZI)
#MjulisheMwingineKuhusuPageHii
#MatajiriWaKesho

No comments:
Post a Comment