Ukiachana na umuhimu wa elimu (SHULE) katika maisha ya binadamu, watu wengi tumeamua kuwekeza katika elimu kuliko sehemu nyingine yoyote. Uwekezaji katika elimu unahusisha miaka yote mtu anayoitumia kutoka shule ya msingi, sekondari, elimu ya juu mpaka muda ambapo mtu atakuwa anafanya kazi. Wawekezaji wengi wa elimu wanategemea kuzalisha pesa nyingi pale watakapoongeza elimu zaidi, mfano mwalimu wa ngazi ya Stashahada (diploma) anapoenda kusoma zaidi ili apate Shahada (Degree) n.k
Kufanya kazi kwa bidii na uaminifu kwa mwajiri wako ni aina nyingine za uwekezaji ambayo pia wengi tumeichagua.Na kupitia hiyo kazi tunapata uhakika wa viinua mgongo hapo baadae na huduma zingine kupitia mikataba yetu na mabosi wetu
Kufanya kazi kwa bidii na uaminifu kwa mwajiri wako ni aina nyingine za uwekezaji ambayo pia wengi tumeichagua.Na kupitia hiyo kazi tunapata uhakika wa viinua mgongo hapo baadae na huduma zingine kupitia mikataba yetu na mabosi wetu
Uwekezaji mwingine ni ule wa kuwa na watoto wengi ili baadae wakuhudumie ukiwa mzee. Kwa bahati mbaya siku hizi maisha yamewaendea mrama watoto wengi kiasi kwamba wameshindwa kuzimudu gharama za maisha na afya za wazazi wao.
Ingawa hiyo iliyotangulia juu ni mifumo mbalimbali ya uwekezaji…uwekezaji mzuri na wa kweli ni ule ambao unakuzalishia kipindi ambacho unaendelea kufanya kazi na sio ule wa kupata pesa zako ukishastaafu. Unataka kuwa mwekezaji wa namna hii..basi jiulize..Je, unaingiza pesa kupitia uwekezaji? Au kwa maneno mengine unaweza kujiuliza..Je, pesa yako inakutumikia na kukuzalishia kipato chako cha sasa hivi?
Tuangalie mfano wa mtu aliyeamua kuwekeza kwa kununua nyumba na kuamua kuipangisha. Kama kodi anayoipokea inazidi gharama za uendeshaji wa ile nyumba basi mtu huyo anaingiza pesa kupitia uwekezaji (eneo I). Au yule ambaye aliamua kununua BODA BODA akampa mtu aendeshe halafu ikawa inazalisha pesa zaidi ya gharama za uendeshaji wake…basi mtu huyo anazalisha pesa kama mwekezaji (TUTASOMA AINA TOFAUTI ZA WAWEKEZAJI). Kwa hiyo ili ujiite MWEKEZAJI (I) ni lazima kuangalia kiasi gani cha pesa unachozalisha eneo lolote (E, S au B) bila ya kufanya kazi katika eneo hilo.

No comments:
Post a Comment