UWEKEZAJI ni jambo muhimu sana ili kuwa na UTAJIRI wa kweli.
Vitu vitano huwatokea ambao hawawekezi au ambao huwekeza bila maarifa ya kutosha:
(i) Hulazimika kufanya kazi maisha yao yote (ii) Wanakuwa na hofu ya pesa maisha yao yote.
(iii) Wanawategemea wengine kama familia, kampuni au serikali katika maisha yao yote.
(iv) Pesa huweka mipaka ya maisha yao ( mf. Siwezi mpeleka mwanangu shule binafsi kwa kuwa sina pesa)
(v) Hawataelewa kamwe nini maana ya uhuru wa kweli (uhuru wa kipesa--utajiri wa kweli)
UNAJIULIZA UWEKEZE KWENYE NINI UFANIKIWE?
Basi unachotakiwa kukifahamu ni kwamba kujiuliza kila siku uwekeze kwenye nini ili ufanikiwe halitakiwi kuwa swali lako tena kuanzia leo. Unachotakiwa kujiuliza ni je, wewe ni mwekezaji mzuri?. Mwekezaji mzuri ni yule ambae ana maarifa ya kutosha juu ya kitu anachokifikiria kuwekeza ikimaanisha kuwa ana ufahamu juu ya mtaji unaohitajika, changamoto zinazoambatana, jinsi ya kuzikabili na mengine mengi.
Hakuna uwekezaji fulani ambao kila atakayeamua kuwekeza eneo hilo atafanikiwa ..hatuoni leo watu fulani wamewekeza katika afya, kilimo, maduka, mitandao ya simu n.k wakafanikiwa sana... lakini kuna wengine tunajaribu humo humo leo kesho lakini hatufanikiwi? Basi jua unachotakiwa ni kutafuta maarifa ya kutosha juu ya kile unachofikiria kukiwekeza. Sidhani kama kuna mtu yeyote hana walau kitu kimoja kichwani kwake anachokifikiria kuwekeza.
Hivi hatujawahi kusikia kuna watu wamejiapiza kabisa kuwa hawatawekeza kamwe kwenye biashara ya nyanya kwa kuwa nyanya huchukua muda mchache sana kuharibika? Na je hatujawaona watu wengine wakiendesha maisha ya familia zao na kuishi vizuri kwa sababu ya biashara hiyo hiyo ya nyanya ambayo yule mwingine ameapa kutoifanya maishani? Hapo ndipo utakapoiona nguvu ya maarifa katika uwezekezaji.
Maarifa juu ya kile unachotaka kukifanya unaweza kuyapata kupitia:
--Kukutana na waliotangulia kufanya kitu hicho
--Kusoma vitabu na majarida mbalimbali
--Kusoma mtandaoni juu ya hiko kitu n.k
#KilaLaKheriTaifaStars
#YouTubeSoon
Tuunge mkono kwa kutembelea

No comments:
Post a Comment