Kama kweli unataka kufanikiwa basi unatakiwa kuondoa HOFU YA KUKATALIWA na pia USIJALI MANENO YA WATU JUU YAKO. Hofu ya kukataliwa inaeleweka sana na wengi kwenye suala la mapenzi ambapo mtu anapohitaji kuwa na mtu fulani kimapenzi anakuwa na hofu kubwa kuwa huenda akakataliwa na mwisho wa siku anaamua aache kueleza ukweli wa moyo wake. Hofu ya kukataliwa inaonekana sehemu nyingi sana na imekuwa ikiwafelisha wengi kufikia ndoto zao...mfano, wengi tunashindwa katika mahojiano (interview) mengi kutokana na kuwa na hofu hii yaani mtu anaanza kutoka jasho kabla hata hajaingia kwenye chumba chenyewe au hata akiingia atakachokiongea hata mwenyewe akitoka nje atashangaa kwa nini imekuwa vile.
Hofu hii hupelekea mambo mengi kama hofu ya kukutana na watu wapya yaani mtu anaona ni kitu kigumu sana kuzungumza na mtu mpya au rafiki wa marafiki zake, na kwa vijana wengi walio vyuoni au maeneo mbalimbali ya elimu huwa na makundi yao yaani marafiki wa aina fulani na inabidi wafanye kama wenzao wanavyofanya hata kama vitu hivyo ni vibaya kwa kuwa wanaogopa huenda wenzao wakawakataa (wanasemaga hauna swaga kama zetu) n.k .
Pia usisahau mambo kama kutaka kuonekana na tabia fulani katika jamii wakati sio ukweli wa tabia yako, kutaka kumridhisha kila mtu, kushindwa kusema unachokihitaji ingawa unakihitaji sana n.k ni baadhi ya tabia zinazoletwa na HOFU YA KUKATALIWA.
USIJALI MTAZAMO/ MANENO YA WATU juu yako yakakusahaulisha ndoto zako. Wengi tunashindwa kufanya vitu tukihofia marafiki watasema nini endapo tutaamua kufanya vitu tofauti. Naomba nitolee mfano wa wanachuo, mwanachuo akipata somo la uwekezaji leo hii na akaamua kubadilika wengi watashindwa kufanikisha suala la uwekezaji na kikubwa zaidi ni maneno ya wenzake kama "huyu jamaa sio mjanja kabisa yaani mavazi yake sio ya kichuo chuo" wakimaanisha kwamba mwanachuo lazima uwe na kiatu kizurii na modo nzuri iliyoshika mwili vilivyo, uwe na unyoaji ambao labda wasanii pekee ndio wananyoa au uwe na suruali inaonyesha mwili ipasavyo au mshono wa kitenge wa kipekee au bei kubwa ambayo huenda hukuwahi kuuwazia kabla hujafika chuo (kwa wanawake) n.k. Basi mambo kama hayo huwafelisha wanachuo na wengine wengi mtaani.
#YoutubeSoon

No comments:
Post a Comment