Leo nimekumbuka ile stori ambayo baba alinisimulia kuwa dada yangu na wanafunzi wenzake walifeli somo la hisabati ingawa walikuwa na mwalimu mzuri (kwao walimuona MBAYA). Baba alidai kuwa dada na wenzake walipeleka ombi kwa mkuu wa shule kuwa hawamtaki mwalimu wao mpya wa Hisabati (Mathematics) kwa kuwa alikuwa akiwachapa sana waliopata maksi chache na alikuwa anapenda kuingia darasani hata kama kipindi sio chake. Mwisho wa stori sikumbuki ilikuwaje kama mwalimu alihama shule au alibadilishiwa kidato ila ninachokumbuka kuwa mwaka aliomaliza dada yangu walifeli sana somo hilo.
Turudi katika mada yetu….MAFANIKIO tunaweza kuyafananisha na huyo mwalimu hapo juu, MAFANIKIO huchapa bakora sana kuliko hata mwalimu aliekua anatuchapa sana bakora tulivyokuwa shuleni. Adhabu ambazo mafanikio yatakutaka uzipitie ni chaguo lako kuzikubali na kuzikabili au kuachana nazo kama ambavyo dada yangu na wanafunzi wenzake walivyofanya.
Ninachokimaanisha hapa ni kwamba tunatakiwa kukubaliana hali kadhalika kukabiliana na changamoto mbalimbali ambazo zitatutokea katika harakati za kutaka kufanikiwa.
Unaweza ukapoteza biashara mbili au tatu kabla ya kupata moja ambayo ikakupa mafanikio na kukusahaulisha shida zako milele. USIKATE TAMAA kama limekutokea hili au kama litakutokea hili katika kupambana kwako. Tunajifunza mengi sana pale tunapofeli kuliko tunapofaulu, kwa hiyo usiogope kufeli.Kufeli ni hatua mojawapo ya mafanikio. Huwezi pata mafanikio bila kufeli.
Tuunge mkono kwa kutembelea... elimuyautajiri.blogspot.com

No comments:
Post a Comment