Kundi hili linaweza kuwa kinyume kabisa na lile la S, watu ambao wamebobea katika kundi B wanapenda kujiweka karibu sana na watu walio vizuri katika maeneo tofauti ya E, S, B na I. Hawa sio kama wale wa S ambao hawapendi kuwapa kazi wengine wakiamini kwamba hakuna anaweza kufanya zaidi yao. B wanapenda kuwapa kazi wengine. Kauli mbiu ya watu hawa ni “KWANINI UFANYE MWENYEWE WAKATI UNAWEZA KUAJIRI WENGINE WAKAFANYA KWA AJIRI YAKO NA WAKAFANYA VIZURI?
UONGOZI MZURI NI SUALA MUHIMU KATIKA ENEO B
“UONGOZI ni ule uwezo wa kumshawishi mtu afanye kazi kwa ubora wake wote alionao”. Uongozi mzuri na maarifa ya biashara ni mambo muhimu sana katika eneo B. Inaonekana wengi wana kitu kimoja kati ya hivyo viwili.. utakuta mtu ana maarifa mazuri tu ya biashara fulani lakini kwa upande wa kuwaongoza watu wake inakuwa tabu au mwingine anajua kuongoza watu vizuri tu lakini hana maarifa ya kutosha ya biashara husika. Ila tambua ili uweze kuwa na mafanikio makubwa katika eneo B lazima uwe na mambo yote mawili na cha kukutia moyo ni kwamba vyote viwili unaweza kujifunza na ukawa vizuri. Maarifa ya uongozi na biashara ni endelevu hayana mwisho kila siku yapasa uendelee kujifunza kutokana na kukutana na watu mbalimbali na pia mabadiliko ya kila siku yanayotokea katika dunia ya leo.
Maarifa kama kusoma taarifa ya biashara, kuangalia masoko ya biashara yako, jinsi ya kuweka makubaliano na wengine, jinsi ya kufanya matangazo ya biashara yako n.k ni mambo ambayo ni rahisi kujifunza. Kwa wengi shida inakuja kwenye suala la kufanya kazi na wengine halafu mambo yakaenda sawa (UONGOZI). UJASIRIAMALI
Wengi tunawasikia wakisema “nataka kuanzisha biashara yangu mwenyewe”. Wengi tunaamini kuwa ili tuwe na uhakika wa pesa na maisha yenye furaha basi inabidi kuanzisha vitu vyetu wenyewe au vitu ambavyo havijawahi fanywa na mtu mwingine yeyote. Wengi tunafanya haraka kuanzisha, ila badala ya kufika kwenye umiliki wa biashara (B) tunaishia kwenye kujiajiri katika biashara hizo (S).

No comments:
Post a Comment