Unaposikia neno kazi yenye uhakika na malipo mazuri, jua maneno haya yanatolewa na mtu mwenye hofu ya kutokuwa na pesa. Yani mwenye mawazo ya ajira mara nyingi ndio yule ambae ana hofu labda kutokuwa na ajira kutamfanya awe na uchumi usioeleweka au huenda akawa maskini asipoajiriwa. Linapokkuja suala la pesa watu wengi huona kama ajira ndo suluhisho kwa kuwa chochote atakachokifanya labda matumizi mabaya au mazuri mwisho wa mwezi lazima nyingine itaingia tu.
Wengi ya waajiriwa wanataka waajiriwe sehemu ambayo itakuwa inawapa huduma kama vile bima na mipango mizuri ya kupata kiinua mgongo pale wakiistaafu.
Jambo muhimu kwa watu hawa ni kuondokana na ile HOFU ya kutokuwa na pesa ifikapo mwisho wa mwezi na wanahitaji kuona uhakika huo ukiwa kwenye maandishi yaani MKATABA. Furaha yao kubwa ni hiyo kazi yenye uhakika, wao suala la uchumi usioeleweka hawataki kulisikia hata kwa bahati mbaya yaani eti ufike mwisho hajui kama atakuwa na hela au laaa? KWAO NI JAMBO GUMU KWELI KWELI. Mara nyingi huwa na msemo unaopita vichwani mwao wakisema, “KAZI YAKO NITAIFANYA KAMA UNAVYOTAKA, ukiniahidi kunifanyia hiki na hiki" .
Wanahitaji kupunguziwa HOFU kwa kiwango fulani au kuondokana kabisa na hofu ya kutokuwa na pesa.... labda na SERIKALI au KAMPUNI fulani.
Pia hawakosei wanaposema hawahitaji kuzalisha pesa nyingi (kuwa MATAJIRI) kwa msemo wao wa “NAIPENDA KAZI YANGU”. Wengi hawaelewi kuwa hii inamaanisha kuwa wameweka kipaumbele uhakika wa kiasi fulani tu cha pesa mwisho wa mwezi kuliko KUZALISHA PESA kwenyewe. Waajiriwa wanaweza kuwa maraisi wa MAKAMPUNI fulani, mhudumu wa ofisi na wengine wengi tunaowafahamu. Wengi hawajali kazi gani wanazozifanya, wanachojali zaidi ni ule UHAKIKA tu wa KIMKATABA kila mwisho wa mwezi.
#KubadilikaKunaanzaNaKujuaWapi Ulipo
#MatajiriWaKesho

No comments:
Post a Comment