Hawa ni wale ambao wazungu wanasema “They want to be their own BOSS” yaani hawahitaji mtu yeyote awapangie suala la pesa wao ndio mabosi kwenye kazi yao, au wale ambao wanahitaji kufanya vitu kipekee yaani hajawahi fanya hivyo mtu mwingine yeyote au wale ambao wanataka kufanya kila kitu wenyewe. Hawa hawapendi kabisa kutegemea watu wengine katika suala pesa na wanataka kulipwa wakimaliza kufanya kazi zao. Hawapendi mtu mwingine awaamulie kiasi cha pesa wanachotakiwa kukipata..hawapendi kuona mtu ambae hajafanya kazi kubwa kama wao anapata pesa zaidi yao. Pia wanafahamu wasipofanya kazi ya maana hawatakiwi kulipwa kiasi kikubwa yaani wanaamini ule msemo “wasipofanya kazi basi na wasile”. VIPI KUHUSU HOFU YA KUKOSA PESA?
Wakati waajiriwa wakijaribu kutoa hofu hiyo kwa kutafuta kazi yenye uhakika wa mshahara, hawa huamua kutoa hofu hiyo kwa kuingia kazini wenyewe na kupambana na kila hali. Katika kundi hili unawakuta wanataaluma mbalimbali ambao wametumia miaka mingi shuleni kama madaktari binafsi, wanasheria au mawakili binafsi n.k. Pia kundi hili linahusisha watu ambao hawajaenda shule kabisa au wale waliokimbia shule kama madalali wakubwa na wadogo, wauza maduka madogo madogo, wafanya usafi, mafundi bomba, seremala, mama ntilie wachungaji, wasusi, mafundi umeme, walimu wa Twisheni wanaofundisha vizuri sana, WASANII n.k.
Nyimbo kubwa wanayoipenda ni ile ya “HAKUNA MTU ANAWEZA ZAIDI YANGU” au “NIMEFANYA KIVYANGU SIO KWA KUIGA”
Wengi ambao wapo katika kundi hili wanazifanya kazi zao vizuri sana yaani hawaamini kama kuna mwingine anaeweza kufanya kama wao na hii ndio maana tunawaajiri kutufanyia kazi zetu.
Nani leo anataka kufanya wayaringi (wiring) nyumbani kwake akamchukua mtu ambae hayuko vizuri katika eneo hilo? Wote tutamtafuta yule fundi ambae alimfanyia vizuri jirani kwa sababu alifanya vizuri. Vipi kuhusu daktari wa meno? Daktari yeyote yule au aliyebobea katika eneo hilo? Na Vipi kuhusu wakili wa kukuendeshea kesi yako? N.k
Kwa watu wa kundi hili PESA sio muhimu sana kuhusu kazi yao, uhuru wa kufanya kazi, pesa ya kutopangiwa na kuheshimiwa kuwa wako vizuri sana katika eneo lao walilobobea ndio mambo wanayoyapa kipaumbele.

No comments:
Post a Comment