elimuyautajiiri.blogspot.com

Monday, July 22, 2019

USIACHE KAZI

                           

HII INAMUHUSU YEYOTE AMBAE AMEAJIRIWA AU ANA NDUGU, RAFIKI YAKE AMEAJIRIWA AU ANATAFUTA AJIRA….. Hakikisha unafikisha elimu hii kwa muhusika

Moja ya tatizo kubwa sana ambalo watu wengi tunakumbana nalo leo hii ni namna gani tunaweza kuwa MATAJIRI. Na katika watu ambao wanapata ugumu zaidi katika kuwaza namna gani wanaweza kuwa MATAJIRI ni wale ambao wameajiriwa. Wengi hujiuliza waache kazi ndo waanze kuutafuta utajiri? Au wafanyaje?. Basi kama nawe ni mmoja wa wale ambao wanajiuliza hivyo @elimu_ya_utajiri inakuambia kabla hujaacha kazi jiulize maswali yafuatayo…. Je una pesa ya kuanzisha biashara? Na kama unazo… una uhakika gani hiyo biashara yako ya kwanza tu itatiki moja kwa moja? Je utakula nini ukiacha hiyo kazi?. Basi tukupe siri tu kuwa unaweza kuendelea na kazi yako na BADO UKAWA TAJIRI. Shida ambayo inawakumba waajiriwa wengi ni kwamba wanatafuta AJIRA wakilenga kupata pesa ambayo itamaliza matatizo yao yote. Kazi pekee haijawahi kumaliza tatizo la pesa…. kama unataka kuwa TAJIRI ni lazima ufanye biashara (mjasirimali) maana biashara pekee ndio ambayo haina ukomo wa mapato… unaweza ukaanza kupata mia leo mpaka kiasi chochote unachokitaka wewe siku moja kutokana na jitihada na malengo yako.

Kama unafanya kazi na bado unasumbuliwa na tatizo la kutokuwa na pesa basi mkombozi wako ni biashara na sio kutafuta kazi nyingine ya ziada. Kamwe huwezi utafuta UTAJIRI ili hali huna unachokiingiza tumboni…USIACHE KAZI. Kama unataka kuwa MJASIRIAMALI WA KWELI basi usifanye kazi kwa ajili ya pesa fanya kazi kwa ajili ya kupata maarifa fulani na uzoefu ambao utakusaidia baadae katika kuusaka utajiri wako. Fanya kazi muda ambao kazi yako inakutaka kuwa ofisini ila ukitoka kazini anza kufanya baishara yako ambayo utalenga kuikuza kila siku na kufikia kupata kipato kikubwa siku moja kuliko kile ambacho unapata kwenye mshahara wako…. KUACHA AU KUTOACHA KAZI SIKU ZA MBELENI BAADA YA BIASHARA YAKO KUANZA KUINGIZA PESA NZURI NI JUKUMU LAKO MWENYEWE. Ila kumbuka tu usifanye kazi sababu ya pesa.


Thursday, July 18, 2019

SHAUKU YA KUFANIKIWA

Kila mtu ambae anafikia umri wa kutambua dhumuni la pesa, anatamani kuwa nazo. Lakini kutamani tu hakumfanyi mtu kuwa TAJIRI. Bali SHAUKU YA KUFANIKIWA ikiambatana na nia ya dhati, kisha ikawepo mipango mikakati thabiti ya kuupata huo UTAJIRI na kuhakikisha hakuna kukata tamaa kwa lolote litakalotokea katika safari hiyo ya mafanikio basi UTAJIRI utapatikana. Anasema maneno hayo Bwana Napoleon Hill katika kitabu chake cha THINK AND GROW RICH 
Anatueleza kuwa njia ambayo SHAUKU YA KUFANIKIWA inaweza kubadilishwa na kuwa mafanikio ya kweli ambayo mtu anayataka (UTAJIRI) ina hatua SITA ambazo zinatekelezeka:
(1) Weka katika akili yako kiwango halisi cha PESA ambacho unataka kukimiliki. Usiseme pesa nyingi… Taja kiwango maalumu (Hii ina maana kubwa sana kisaikolojia, tutaelezana siku za mbeleni)
(2) Bainisha kinagaubaga namna gani utajitoa kuhakikisha unafikia malengo yako ya kumiliki hizo pesa. Mf. Kama malengo yako yatakuhitaji uwe bize walau siku nzima au  muda mwingine kuahirisha baadhi ya starehe zako basi uko tayari nk
(3)Weka muda maalumu ambao unataka kumiliki hizo pesa. Mf. Baada ya miaka mingapi? Miezi mingapi? Nk
(4)Weka mipango mikakati thabiti ambayo itakupelekea kufikia hayo malengo yako na ANZA KUTEKELEZA MARA MOJA… haijalishi uko tayari au hauko tayari kutekeleza.
(5)Andika vizuri kiasi cha pesa unachohitaji kukimiliki, muda wa mwisho ambao unatakiwa uwe umefikia lengo lako, elezea namna ambayo uko tayari kujitoa kwa ajili ya lengo lako, na elezea kwa kirefu mpango mkakati wako ambao utakupelekea  kuzipata hizo pesa. ( HAPA PANAHUSISHA KUANDIKA)
(6)Soma maelezo yako utakayoyaandika kwa sauti ya kawaida (sio kwa kunong’ona), mara mbili kwa siku, kabla hujalala usiku na unapoamka tu asubuhi. Na unaposoma…ona, hisi na kuamini kana kwamba tayari unazimiliki hizo pesa. (KUAMINI NA KUJIONA TAYARI UNAZIMILIKI HIZO PESA NI JAMBO MUHIMU ZAIDI)

USHAURI WA MTAZAMO WA KITAJIRI
Katika kufikiria kiwango cha pesa unachotaka kumiliki…..Kama UMEJIAJIRI AU UMEAJIRIWA…. Jiwekee malengo ya baada ya muda gani uwe una MZUNGUKO WA PESA UNAOUHITAJI (CASH FLOW) kwa mwezi kutoka vyanzo vyako mbalimbali ambavyo unataka kuvimiliki na ambavyo vitaingiza hiyo PESA bila uwepo wako kabisa au ushiriki wako mdogo. Mfano, unaweza sema baada ya miaka mitano nitataka niwe na MZUNGUKO WA PESA wa sh. LAKI TATU bila mimi kuwepo kwenye vyanzo hivyo halafu weka mikakati na kuanza kuitekeleza. Hii itawasaidia WAAJIRIWA na WALIOJIAJIRI kufikia UTAJIRI wa kweli siku moja na sio tu kutegemea mshahara maisha yote. SAFARI NJEMA KWAKO AMBAE UTATEKELEZA…..



Face the challenge