(1) Mwekezaji daraja la 4 anatumia pesa yake kuwekeza ila Mwekezaji namba 5 anatumia pesa za watu wengine kuwekeza (kwa kuwa namba 5 anamiliki Biashara kubwa faida anayoipata ndio anayoitumia kuwekeza)
Na hii ndio tofauti kubwa kati ya wawekezaji hawa wawili. (2) Mwekezaji namba 4 anawekeza huku akiamini yeye ndio bora zaidi,
Mwekezaji namba 5 anawekeza huku akiamini katika ushirikiano wa wengine. Hii ikimaanisha kuwa sio lazima yeye ndiyo awe bora zaidi kuliko wengine bali timu yake kwa ujumla ndiyo iwe bora zaidi. Wengi wetu tunaamini kuwa kuwa vichwa viwili ni bora kuliko kichwa kimoja lakini wengi pia bado tunaendelea kuamini kuwa sisi ni bora kuliko watu wote. (kama bado unajiona hivi jua wewe ni MWEKEZAJI DARAJA LA NNE) (3) Mwekezaji namba 4 anazalisha pesa chache ukilinganisha na mwekezaji nambari 5. (4) Mwekezaji namba 4 pia anasimama kama mtu MBINAFSI na jinsi anavyozidi kuwa mbinafsi ndio jinsi anavyotengeneza pesa zaidi. Tuchukulie mfano wa MC mzuri wa sherehe …unajua ili atengeneze pesa nyingi iweje? Inabidi apate madili mengi zaidi, sasa chukulia kapata madili 10…akimstua mwingine afanye walau mawili kati ya hayo kumi si pesa kwake inapungua??? Kama sio UBINAFSI ni nini huo?
Mwekezaji namba 5 anasimama kama mtu MKARIMU, jinsi anavyokuwa mkarimu ndio jinsi pesa inavyoingia zaidi. Mtu kukupa kazi tutauchukulia kama UKARIMU sio? Tunamsemeaje mtu anayefanya biashara ya duka na kila linapokua anafungua sehemu nyingine na kumuweka mtu….Hii haimaanshi kila anapokuwa MKARIMU zaidi basi na pesa inaingia zaidi??? (5) Ni ngumu kukuza mtaji ukiwa na MTAZAMO KAMA WA MWEKEZAJI DARAJA LA NNE (mf. Lazima niwepo mimi mwenyewe ili biashara iende vizuri, akikaa mwngine mambo hayaendi vizuri). Na ni rahisi sana kukuza mtaji ukiwa na mtazamo wa mwekezaji namba TANO (mf. Hili duka langu likikua nitafungua lingine sehemu fulani halafu nitamuweka fulani sio lazima niwe mimi ili biashara iende vizuri). Mtu akifahamu tu namna ya kuifanya biashara yake ikawa kubwa basi mafanikio hayo yataleta pesa nyingi zaidi. Inakuwa rahisi sana kutengeneza pesa kupitia UWEKEZAJI kama utafanikiwa kuikuza biashara yako ikawa kubwa.
Usisahau kutembelea

No comments:
Post a Comment