MATAJIRI HAWAITUMIKII PESA, WANAITUMIKISHA PESA
Hivi unajisikiaje kupanga mstari kusubiria pesa ya siku? au unajisikiaje pale tarehe uliyotegemea mshahara utoke na haukutoka? au unajisikiaje kuamka kila siku asubuhi na mapemaa kuwahi kibaruani ulipojiajiri na kurudi usiku nyumba nzima imelala? n.k
Endapo vitu kama hivi bado vinakutokea katika maisha yako...nikuambie tu ukweli kuwa unaitumikia pesa..ila nikupe moyo tu kuwa HAIMAANISHI kwamba hautaweza kamwe kuitumikisha pesa kama utaamua kubadilika leo hii ukawa na mtazamo wa kiTAJIRI.
Tunaambiana kila siku na tutaendelea kuambiana kuwa tujifunze kuitumikishe pesa sio kuitumikia milele. Muhimu kufahamu kwamba kusoma kuitumikisha pesa ni jambo ngumu linalohitaji utayari wa mtu binafsi na nia ya kuondokana na kizazi cha kimaskini.
KWANINI NI NGUMU KUSOMA KUITUMIKISHA PESA?
Ni ngumu kwa sababu kuitumikisha pesa kunahusisha kufahamu changamoto mbalimbali zinazotokea katika kuwekeza na kukubali kuzikabili, uthubutu na msimamo wa kulisimamia jambo uliloliamua, utayari wa kupata funzo pale utakapofeli n.k. Wengi wetu hatuna vitu hivi zaidi tumejawa na mawazo hasi...badala ya kujengwa na changamoto sisi zinakuwa sababu ya kukata tamaa. Mfano, kama kuna mtu aliamua kuwekeza katika korosho msimu huu na matokeo yake msimu haujaenda vizuri kama ilivyozoeleka. Wengi walioanza kuwekeza katika zao hilo msimu huu ni wachache tu kati yao watakaoamua kuwekeza tena mwakani. WENGI WAMESHAAGANA NA ZAO HILO.....kifupi changamoto hazijawajenga...zimewakatisha TAMAA
KWANINI NI RAHISI KUSOMA KUITUMIKIA PESA?
Kwanza kinachotufanya wengi tuamue kuitumikia pesa ni kutoka na HOFU. Wengi tunajiuliza:
Je, nikiweka pale pesa yangu..isipozalisha?? si ishakula kwangu
Nianze moja? nikishindwa kulipa kodi ya nyumba?
Kwa hiyo wengi tunaamua kwenda kuajiriwa mahali Fulani tupate mshahara tupate uhakika wa kodi na mengine mengi huku tukijisahau kupambana kuitumikisha pesa siku moja. Lakini wengi tunaofanya maamuzi hayo ya kupata uhakika wa kodi tunaendelea kushangaa kwa nini matatizo ya pesa HAYAISHI.
Tunasahau kuwa tatizo ni kukosa elimu ya kuitumikisha pesa (elimu ya pesa @elimu_ya_utajiri). Chagua leo kuitumikia au kuitumikisha PESA.

No comments:
Post a Comment