Hiyo picha inayoonekana hapo juu ni kitu ambacho bwana Robert Kiyosaki anakiita CASHFLOW QUADRANTS tunaweza kuita JEDWALI LA MZUNGUKO WA PESA ...huu ni mgawanyo ambao unaonyesha maeneo mbalimbali ambapo tunazalisha pesa zetu.
E inawakilisha watu ambao wanaingiza pesa kupitia AJIRA (EMPLOYEE)
S inawakilisha watu ambao wanaingiza pesa kupitia biashara ndogo ndogo au kupitia kujiajiri kwao (SMALL BUSINESS au SELF EMPLOYED)
B inawakilisha watu wanaoingiza pesa kupitia biashara kubwa (BIG BUSINESS/BUSINESS OWNERS)
I inawakilisha wawekezaji (INVESTORS)- hapa pesa inazalisha pesa zaidi
Jedwali hili la mzunguko wa pesa bwana Robert Kiyosaki anajaribu kutuonyesha wapi tulipo na kutupa muongozo wa wapi inatakiwa tuwepo ili kufikia UTAJIRI WA UKWELI (utajiri ambao utafika hatua ambayo sio lazima kufanya kazi, kufanya au kutofanya ni maamuzi yako lakini unaishi vizuri na pesa zinazidi kuingia na kuongezeka). Anatuambia kuwa UTAJIRI huo unaweza kupatikana popote pale utakapokuwa katika mzunguko huo ila ukiwa na elimu ya B na I itakusaidia kufikia malengo hayo kwa haraka zaidi
Kaa tayari nitakufikishia elimu hapahapa....elimu ambayo itakusaidia kutoka upande wa kushoto wa E na S kwenda upande wa kulia wa B na I. Cha kusisitizia tu kuwa elimu hii ni kwa wale tu ambao wako tayari kutoka kwenye kuitumikia pesa mpaka kwenye kuitumikisha pesa. Sio kazi rahisi kufikia ila ina thamani ya kuipambania elimu hii na kuitumia kama mwongozo katika maisha yako ya kila siku.....
# MjulisheNaMwingineKamaUnampend a
#MjulisheAnayeutakaUtajiri.

No comments:
Post a Comment