Inawezekana kutengeneza pesa katika eneo lolote la JEDWALI LA MZUNGUKO WA PESA...pia inawezekana kutengeneza pesa kupitia maeneo yote pia, kumbuka kuzalisha pesa katika maeneo yote hiahusiaini na elimu inayopatikana darasani Bali inategemea utayari wa mtu, kujua madhaifu yako na sehemu gani uko vizuri.
Utofauti uliopo kati yetu binadamu unatutofautisha katika maeneo ya kuzalisha pesa..mfano, kuna mwingine anapenda sana kuajiriwa ila kuna mwingine hataki hata hata kusikia habari za kuajiriwa...
kuna mtu anapenda kumiliki biashara fulani lakini hapendi kuiendesha mwenyewe... na mwingine anapenda kumiliki biashara hiyo na kuiendesha pia, kuna mwingine anapenda kuwekeza lakini mwingine anaogopa sana hasara (changamoto) ambazo ni sehemu ya kuwekeza...Usijali popote pale unaweza kuwa TAJIRI ni wewe tu. Mfano, mtu yeyote aliyeajiriwa anaweza ingiza pesa kupitia biashara ndogo ndogo au kubwa.
Kuwa katika eneo Fulani hakugarantii mafanikio yako..mfano, kujiajiri...wengi wamejiajiri katika biashara fulani au kazi fulani kama seremala mama Ntilie n.k lakini wangapi ni matajiri? tatizo ni sisi wenyewe. (tuna mengi ya kuyaongea hapa na ndio sababu iliyonituma mimi niwafikishe elimu hii watanzania wengi ambao TUMEAMUA KUJIAJIRI-kujiajiri tu sio suluhisho @elimu_ya_utajiri jumlisha kujiajiri ndio SULUHISHO)
Inachotakiwa kujua uko wapi na wapi unataka kufika, unahitajika kupata elimu ya eneo ulipo na eneo unalohitaji kufika siku moja. Ila bwana Robert Kiyosaki yeye anatuambia alichagua kuingiza pesa kupitia B na I kwa sababu aliona katika biashara kubwa na kuwekeza hakuna kodi na makato mengi. Kwahiyo kila siku alipambana kufika huko mpaka akafanikiwa...Anasema kwa kupambana kuzalisha pesa siku moja kupitia B na I kutakuwezesha kutengeneza pesa kwa haraka na pia kufanya pesa ikutumikie siku moja kama yeye alivyofanya.
JEDWALI LA MZUNGUKO WA PESA ni muhimu sana kwa kuwa linakuelezea na kukuonyesha njia mbalimbali ambazo pesa inazalishwa. Pia anatuweka wazi njia ambazo tunaweza kuzalisha pesa bila kutoa jasho kubwa. Anazidi kutusisitizia kuwa kama tunahitaji kuzalisha pesa katika eneo fulani lazima tuwe na elimu jinsi mambo yanavyoenda katika eneo hilo.

No comments:
Post a Comment