Hawa ni wale ambao wanahisi wanaweza kufanya kila kitu wenyewe, wengi ya waliostaafu huingia katika daraja hili pindi muda wao wa kufanya kazi unapoisha. Mfano kama anataka kuwekeza katika jambo fulani kila kitu atafanya yeye mwenyewe kama kufanya utafiti wa eneo zuri la kufanya uwekezaji wake, kutafuta wateja, kufanya marekebisho yoyote, gharama zozote zile ataingia kwa pesa zake n.k
Mara nyingi watu ambao wanahisi wanaweza kufanya kila kitu wenyewe wanakuwaga na elimu ndogo kuhusiana na mambo ya pesa. Na hata wakipata nafasi ya kupata elimu basi wanaegemea katika eneo husika wanalolipenda kupitia kozi moja au mbili.
Jua kwamba hili daraja sio tu kwa wastaafu bali ni daraja ambalo watu wengi tunaopata mawazo ya kuwekeza tunaangukia..... yaani wengi tunawekeza lakini katika uwekezaji wetu wengi tunaona kila kitu tunaweza kufanya wenyewe au mpaka tuwepo wenyewe ndipo mambo yatakapoenda vizuri zaidi.
Huku wengine wakisema kuwa hakuna anayeweza kufanya vizuri zaidi ya wanavyofanya wao yaani tunajiona ni wa kipekee zaidi katika eneo letu fulani tulilobobea tukisahau kwamba kuwaza hivyo kunatuchelewesha kuwa MATAJIRI wa kweli.
Usisahau kutusapoti kwa kutembelea

No comments:
Post a Comment