Hawa ni wawekezaji pia ila ni wale ambao wako bize sana kiasi cha kuona kuwa hawana muda wa kujifunza UWEKEZAJI. Wengi ambao wako katika hili daraja ni wale waliosoma sana yaani wako bize na kazi zao (taaluma walizomea), familia au vitu vingine wanavyovipendelea hali kadhalika likizo wanazokuwa nazo kila baada ya muda fulani. Kwa hiyo kutokana ubize wao wanaona haina haja ya kujifunza uwekezaji na kuamua kuwakabidhi wengine wawafanyie huo uwekezaji. Mara nyingi wanawapa watu waliobobea katika eneo fulani wawawekezee huku wakibaki kusali na kuomba usiku na mchana kuwa yule waliyemkabidhi aendeshe mambo vizuri.
Tatizo kubwa linaloambatana na hili daraja ni kwamba pale mtu atakapopoteza pesa au kupata hasara ya kiwango fulani hana anachojifunza. Hawapati somo lolote zaidi tu ya kupata somo baya kwamba usiwekeze kwenye jambo fulani utapoteza pesa zako bure. Ambacho watafanya zaidi ni kumlaumu yule jamaa waliyemkabidhi pesa, kulaumu soko au serikali (kwa jinsi inavyobadilisha kiwango cha kuwapa viinua mgongo vyao kwa wale walioajiriwa---hawa wamewapa serikali wawatunzie pesa). Fahamu kwamba ni ngumu kujifunza umekosea wapi kama hujui kosa gani limefanyika.
#YouTubeSoon
Tembelea BLOG yetu kutuunga mkono... elimuyautajiri.blogspot.com

No comments:
Post a Comment