elimuyautajiiri.blogspot.com
Tuesday, May 21, 2019
Thursday, May 9, 2019
SOMO LA AROBAINI
Watu wengi wanaamini kutengeneza pesa nyingi zaidi kutatatua matatizo yao yote ya pesa. Ila mara nyingi husababisha matatizo makubwa zaidi. Moja ya sababu kubwa inayosababisha matatizo mengi ya pesa kwa watu ni kwamba hawajawahi kufundishwa jinsi ya kudhibiti mzunguko wao wa pesa. Wamefundishwa kujua kusoma, kuandika, kuendesha gari nk lakini sio namna ya kudhibiti mzunguko wao wa pesa. Bila ya kulijua hili wanaishia kuwa na matatizo ya pesa kila kukicha na kuendelea kufanya kazi kwa bidii zaidi wakiamini kwamba kutengeneza pesa nyingi zaidi kutamaliza matatizo yao. JUA KWAMBA PESA NYINGI HAZITAMALIZA MATATIZO YAKO YA PESA KAMA UKISHINDWA KUDHIBITI MZUNGUKO WAKO WA PESA. Pesa nyingi zaidi huwafanya watu wengi kuwa maskini kwa sababu huongeza matumizi na kuangukia kwenye madeni makubwa kila mara wanapoongezwa mshahara.
Unatakiwa ukae chini uweke mpango wa kudhibiti matumizi na kupunguza madeni hali kadhalika kupunguza vitu ambavyo vinakupunguzia pesa mfukoni. Nimekuandalia hapa chini namna ambayo itakuwezesha kudhibiti mzunguko wako wa pesa.
Ila fanya hivi kabla sijakuambia:
(1) Ainisha kipato chako na matumizi yako kwa mwezi.
(2) Angalia eneo ambalo unazalisha kipato chako (mwajiriwa, umejiajiri, mmiliki wa biashara au mwekezaji)------Kumbuka mmiliki wa biashara ni yule ambaye anaweza akaondoka mbali na biashara yake hata mwaka au miaka miwili lakini akakuta biashara yake bado ipo au imekuwa zaidi. Ukiona huwezi kufanya hivyo basi jua umejipa kazi mwenyewe/ umejiajiri
(3) Ainisha eneo gani ambalo unataka kuzalisha pesa nyingi zaid baada ya miaka mitano (Baada ya miaka mitano unataka kuzalisha pesa nyingi kama mwajiriwa, aliyejiajiajiri, mmiliki wa biashara au mwekezaji?)
Haya sasa baada ya kufanya hivyo uko tayari kuanza mpango mkakati wa kudhibiti mzunguko wa pesa. Ni hatua mbili tu za kuzifanya:
(1) Jilipe mwenyewe kwanza
Tenga asilimia fulani kila unapopata kipato au mshahara wako kwa ajili ya kuwekeza. Na ukikitunza usikitoe ulipokitunza mf. Benki mpaka pale utakapoona kuwa uko tayari kuwekeza.
(2) Lipa deni
Kama una madeni basi tenga asilimia nyingine kwa ajili ya kulipa deni mpaka libakie sifuri na uongeze hiyo asilimia uliyoweka kulipa deni lako la mwisho kwa ajili ya kuwekeza. Na hakikisha kipindi unalipa deni usiongeze deni lingine.
Wednesday, May 8, 2019
MUNGU NA UWEKEZAJI (SOMO LA 1)
SOMO JIPYA LA ELIMU YA UTAJIRI
KUHUSU MUNGU NA UWEKEZAJI
NA MADAM FAITH
KARIBU SANA
Friday, May 3, 2019
SOMO LA THELATHINI NA TISA
Umekuwa ukijiuliza kuwa unawezaje kuwa MMILIKI WA BIASHARA na MWEKEZAJI mwenye mafanikio?....Basi hatua saba zifuatazo zitakupa muongozo kufikia hapo: (1) JALI MAMBO/ BIASHARA YAKO
Hii tutaiongelea kipesa zaidi sio kama wengi wanavyotafsiri. Kiufupi tunasema usiwafanye wengine kuwa MATAJIRI ukajisahau wewe. Jifanye kuwa TAJIRI. (2) DHIBITI MZUNGUKO WAKO WA PESA
Usipoweza kudhibiti mzunguko wako wa pesa basi kupata nyingi zaidi hakutakufanya kuwa TAJIRI (3) TAMBUA TOFAUTI KATI YA KITU KINACHOHITAJI UJASIRI KUKIFANYA NA KITU HATARI KUKIFANYA
Biashara na uwekezaji si vitu hatari kuvifanya bali kutokuwa na elimu ya pesa (kutojua mzunguko wa pesa ukoje) ni hatari. (4) AMUA MWEKEZAJI WA AINA GANI UNATAKA KUWA
Tutaongelea aina tatu zingine za wawekezaji. Unatakiwa kuanza kidogo kidogo huku ukijifunza kutatua matatizo mbalimbali ya pesa yanayowakumba watu. (5) TAFUTA MWALIMU/ MSHAURI WAKO (MENTOR)
Mshauri/ mwalimu ni mtu anayekuambia kipi ni muhimu na kipi si muhimu. (6) USIVUNJIKE MOYO/ USIKATE TAMAA
Jiandae kukatishwa tamaa. Tumia kukosa kwako tumaini kama motisha wa kuamka na kupambana tena. (7) JIAMINI KATIKA KILE UNACHOKIFANYA
Pesa haikai kwa watu ambao hawajiamini katika harakati zao.
Tutakuchambulia hapa hapa moja baada ya nyingine. TURN ON POST NOTIFICATIONS
Wale waliokuwa wanataka group la whatsapp la @elimu_ya_utajiri link ipo kwenye BIO...JIUNGE
Thursday, May 2, 2019
SOMO LA THELATHINI NA NANE
Ushawahi sikia mtu anafanya kazi kwa bidii na badala ya kuwa TAJIRI anafanya wengine wawe MATAJIRI?
Tangu hapo zamani binadamu tumekuwa tukijali sana mambo ya watu wengine na kuwafanya kuwa MATAJIRI tukisahau mambo yetu. Hili huanza kwa maneno mazuri sana ya ushauri kama:
1. “Nenda shule na hakikisha unapata ufaulu wa juu ili upate kazi yenye mshahara mkubwa”
Tangu hapo zamani binadamu tumekuwa tukijali sana mambo ya watu wengine na kuwafanya kuwa MATAJIRI tukisahau mambo yetu. Hili huanza kwa maneno mazuri sana ya ushauri kama:
1. “Nenda shule na hakikisha unapata ufaulu wa juu ili upate kazi yenye mshahara mkubwa”
2. “ Fanya kazi kwa bidii ili ununue au ujenge nyumba ya ndoto zako. Nyumba yako ni hazina kubwa sana kwako na ni uwekezaji muhimu kuliko wote”
Watu ambao hufuata ushauri huu bila kufikiri mara nyingi huishia kuwa:
1. Waajiriwa, huwafanya maboss na waajiri wao kuwa matajiri.
1. Waajiriwa, huwafanya maboss na waajiri wao kuwa matajiri.
2. Wadaiwa, hufanya benki na wakopeshaji kuwa matajiri.
3. Mtumiaji mkubwa wa vitu vya watu (consumer), huwafanya wamiliki wa biashara kuwa matajiri. (wengi ya waajiriwa hawamiliki biashara yoyote). Yaani hawa badala ya kuhangaika namna gani wanakuwa matajiri, wanawafanya wengine wote kuwa matajiri kasoro wao. Badala ya kujali mambo/ biashara yao wanajali ya wengine, hufanya kazi maisha yao yote kuwafanya wengine kuwa matajiri. Na ukiangalia mustakabali wa maisha yao utaona kupitia MSHAHARA anajali biashara au mambo ya boss wake na kupitia MATUMIZI yake ya kila siku anajali biashara za watu wengine YAKE WALA HANA HABARI NAYO mana hana biashara yoyote inayomuingizia hela zaidi ya MSHAHARA wake na akipata mshahara wote utaishia kwenye matumizi akijua mwingine utakuja mwisho wa mwezi.
Na yule mwingine asiyeajiriwa ana biashara lakini miaka nenda rudi haikui maana yake ni kwamba anajali biashara za wengine kupitia MATUMIZI (expenses) yake yaani akitengeneza pesa(income/ kipato) tu karibu yote inaishia kwenye matumizi hawazi kuhusu kukuza BIASHARA yake. Wengi hali zetu za kiuchumi zinasikitisha kwa kweli sijajua kinachoendelea kwenye vichwa vya wengine lakini naamini huenda kwa kuwa hatujapata ushauri au elimu sahihi, sasa mimi nimekupa @elimu_ya_utajiri usiseme tatizo hukupata elimu sahihi. Nakwambia kuanzia sasa anza KUJALI MAMBO/ BIASHARA YAKO kama kweli unataka kuwa mmiliki wa biashara na mwekezaji mwenye mafanikio (TAJIRI).
#RipDrReginaldMengi
Na yule mwingine asiyeajiriwa ana biashara lakini miaka nenda rudi haikui maana yake ni kwamba anajali biashara za wengine kupitia MATUMIZI (expenses) yake yaani akitengeneza pesa(income/ kipato) tu karibu yote inaishia kwenye matumizi hawazi kuhusu kukuza BIASHARA yake. Wengi hali zetu za kiuchumi zinasikitisha kwa kweli sijajua kinachoendelea kwenye vichwa vya wengine lakini naamini huenda kwa kuwa hatujapata ushauri au elimu sahihi, sasa mimi nimekupa @elimu_ya_utajiri usiseme tatizo hukupata elimu sahihi. Nakwambia kuanzia sasa anza KUJALI MAMBO/ BIASHARA YAKO kama kweli unataka kuwa mmiliki wa biashara na mwekezaji mwenye mafanikio (TAJIRI).
#RipDrReginaldMengi
Whatsapp group link ipo kwenye BIO
Subscribe to:
Comments (Atom)
-
Kila mtu ambae anafikia umri wa kutambua dhumuni la pesa, anatamani kuwa nazo. Lakini kutamani tu hakumfanyi mtu kuwa TAJIRI. Bali SHAU...


