elimuyautajiiri.blogspot.com

Friday, May 3, 2019

SOMO LA THELATHINI NA TISA

Umekuwa ukijiuliza kuwa unawezaje  kuwa MMILIKI WA BIASHARA na MWEKEZAJI mwenye mafanikio?....Basi hatua saba zifuatazo zitakupa muongozo kufikia hapo: (1) JALI MAMBO/ BIASHARA YAKO 

Hii tutaiongelea kipesa zaidi sio kama wengi wanavyotafsiri. Kiufupi tunasema usiwafanye wengine kuwa MATAJIRI ukajisahau wewe. Jifanye kuwa TAJIRI. (2) DHIBITI MZUNGUKO WAKO WA PESA
Usipoweza kudhibiti mzunguko wako wa pesa basi kupata nyingi zaidi hakutakufanya kuwa TAJIRI (3) TAMBUA TOFAUTI KATI YA KITU KINACHOHITAJI UJASIRI KUKIFANYA NA KITU HATARI KUKIFANYA
Biashara na uwekezaji si vitu hatari kuvifanya bali kutokuwa na elimu ya pesa (kutojua mzunguko wa pesa ukoje) ni hatari. (4) AMUA MWEKEZAJI WA AINA GANI UNATAKA KUWA
Tutaongelea aina tatu zingine za wawekezaji. Unatakiwa kuanza kidogo kidogo huku ukijifunza kutatua matatizo mbalimbali ya pesa yanayowakumba watu. (5) TAFUTA MWALIMU/ MSHAURI WAKO (MENTOR)
Mshauri/ mwalimu ni mtu anayekuambia kipi ni muhimu na kipi si muhimu. (6) USIVUNJIKE MOYO/ USIKATE TAMAA
Jiandae kukatishwa tamaa. Tumia kukosa kwako tumaini kama motisha wa kuamka na kupambana tena. (7) JIAMINI KATIKA KILE UNACHOKIFANYA
Pesa haikai kwa watu ambao hawajiamini katika harakati zao.

Tutakuchambulia hapa hapa moja baada ya nyingine. TURN ON POST NOTIFICATIONS
Wale waliokuwa wanataka group la whatsapp la @elimu_ya_utajiri link ipo kwenye BIO...JIUNGE

No comments:

Post a Comment

Face the challenge