elimuyautajiiri.blogspot.com

Thursday, May 2, 2019

SOMO LA THELATHINI NA NANE





Ushawahi sikia mtu anafanya kazi kwa bidii na badala ya kuwa TAJIRI anafanya wengine wawe MATAJIRI?
Tangu hapo zamani binadamu tumekuwa tukijali sana mambo ya watu wengine na kuwafanya kuwa MATAJIRI tukisahau mambo yetu. Hili huanza kwa maneno  mazuri sana ya ushauri kama:
1. “Nenda shule na hakikisha unapata ufaulu wa juu ili upate kazi yenye mshahara mkubwa”
2. “ Fanya kazi kwa bidii ili ununue au ujenge nyumba ya ndoto zako. Nyumba yako ni hazina kubwa sana kwako na ni uwekezaji muhimu kuliko wote”
Watu ambao hufuata ushauri huu bila kufikiri mara nyingi huishia kuwa:
1. Waajiriwa, huwafanya maboss na waajiri wao kuwa matajiri.
2. Wadaiwa, hufanya benki na wakopeshaji kuwa matajiri.
3. Mtumiaji mkubwa wa vitu vya watu (consumer), huwafanya wamiliki wa biashara kuwa matajiri. (wengi  ya waajiriwa hawamiliki biashara yoyote). Yaani hawa badala ya kuhangaika namna gani wanakuwa matajiri, wanawafanya wengine wote kuwa matajiri kasoro wao. Badala ya kujali mambo/ biashara yao wanajali ya wengine, hufanya kazi maisha yao yote kuwafanya wengine kuwa matajiri. Na ukiangalia mustakabali wa maisha yao utaona kupitia MSHAHARA anajali biashara au mambo ya boss wake na kupitia MATUMIZI yake ya kila siku anajali biashara za watu wengine YAKE WALA HANA HABARI NAYO mana hana biashara yoyote inayomuingizia hela zaidi ya MSHAHARA wake na akipata mshahara wote utaishia kwenye matumizi akijua mwingine utakuja mwisho wa mwezi.
Na yule mwingine asiyeajiriwa ana biashara lakini miaka nenda rudi haikui maana yake ni kwamba anajali biashara za wengine kupitia MATUMIZI (expenses) yake yaani akitengeneza pesa(income/ kipato) tu karibu yote inaishia kwenye matumizi hawazi kuhusu kukuza BIASHARA yake. Wengi hali zetu za kiuchumi zinasikitisha kwa kweli sijajua kinachoendelea kwenye vichwa vya wengine lakini naamini huenda kwa kuwa hatujapata ushauri au elimu sahihi, sasa mimi nimekupa @elimu_ya_utajiri usiseme tatizo hukupata elimu sahihi. Nakwambia kuanzia sasa anza KUJALI MAMBO/ BIASHARA YAKO kama kweli unataka kuwa mmiliki wa biashara na mwekezaji mwenye mafanikio (TAJIRI).
#RipDrReginaldMengi
Whatsapp group link ipo kwenye BIO

























No comments:

Post a Comment

Face the challenge