elimuyautajiiri.blogspot.com

Wednesday, April 24, 2019

SOMO LA THELATHINI NA SABA



Leo tuongee kidogo kuhusiana na UHURU WA KUCHAGUA. Hakuna uhuru mkubwa zaidi ya kuishi utakavyo. Mara nyingi tumezoea wazazi wakijaribu kila namna ili watoto wao waishi namna ambavyo wanataka hususani katika masuala ya AJIRA yaani wazazi wengi wanatamani watoto wao wawe madaktari, mainjinia, wanajeshi nk 

Mwanzoni watoto hujitahidi kufanya kama wazazi wanavyotaka ila Kuna wakati unafika mtu anaamua kuishi yeye anavyohitaji sio tena kama ambavyo vile wazazi wao walivyoishi au walivyohitaji yeye aishi. Huenda familia yake iliishi kwa kutegemea mshahara ila yeye akaamua kutoishi ivo labda kwa kuwa aliona wazazi wake wakihangaika kila mwezi kuhakikisha mshahara wa mwezi huu unakutana na mshahara wa mwezi ujao. Hili huenda sio suala la kuwaumiza kichwa watu wengi, huenda wakawa wameyachagua maisha  hayo na kuyapenda tusigombane mana huo ndio UHURU WA KUCHAGUA ingawa kujaribu kuelimishana ni muhimu ila tunapaswa kuheshimu CHAGUO LA MTU ni maisha yake na yuko huru kuchagua.

Kuna watu wanapenda kuishi katika mfumo ambao mshahara wake kila mwaka unapanda daraja au anapanda cheo ila kuna watu hawataki kupitia njia hiyo. Kuna watu wanataka kuwa na ujuzi wa kipekee zaidi akijiajiri katika fani fulani, kuna wengine hawataki kusikia na hawajayachagua maisha hayo. Haishauriwi wote tufate njia kama aliyepita fulani HAPANA. Chagua njia unayoitaka na kuipenda halafu pita hiyo. Narudia tena ni CHAGUO LAKO , ISHI UNAVYOTAKA 

Kuna wengine wamesoma mpaka chuo kikuu na wakafika hatua wakaona kuwa kuendelea kutafuta shahada zingine sio jambo ambalo wao wamelichagua. Huenda wameona kuwa shule haifanyi watu kuwa matajiri maana ana ushahidi wa watu wengi waliosoma sana na sio MATAJIRI na yeye amechagua kuwa TAJIRI. 
Chagua njia unayoipenda na unahisi itakuletea furaha halafu pita. #IshiUtakavyoUsivunjeSheriaZaNchi#TusimsahauMungu
#SisiTumechaguaKuwaMATAJIRI

No comments:

Post a Comment

Face the challenge