Wengi ambao tunaamua kujiajiri mara nyingi hupenda kama sio kulazimika kwa kuanza na biashara ndogo ndogo. Katika biashara hizo huwa tunajitahidi kuwa kila kitu ili biashara isonge mbele kama vile kujibu simu zinazopigwa na wateja, kulipia bili mbalimbali, kupiga simu, kujaribu kutangaza biashara kwa bajeti ndogo, kuwahudumia wateja, kufukuza kazi wasaidizi wetu tunaoona wanafanya ovyo, kuwaajiri wasaidizi wengine, kuchukua nafasi ya wasaidizi wetu kama hawajatokea siku fulani ya kazi n.k...mfano mzuri unaweza kuwa mama ntilie, waliojiajiri kwa kufungua duka na wengine wengi.
Hivi ujawahi kusikia kijana fulani aliwekeza wekeza na kuazima kwa ndugu zake kiasi fulani cha pesa ili kimsapoti katika kuanzisha biashara yake mwenyewe halafu baada ya miaka mitatu au zaidi biashara ikaanza kwenda ovyo na badala ya kufanikiwa (kutoboa) kama alivyowambia wenzake...... anabaki na deni?
Unaambiwa biashara 9 kati ya 10 za namna hii hufeli baada ya miaka mitano. Na zile zilizofanikiwa kubaki 9 katika ya 10 hufeli baada ya miaka mitano mingine. Kifupi biashara 99 kati ya biashara ndogo ndogo 100 hufeli baada ya miaka 10.
Wengi hufeli ndani ya miaka mitano ya kwanza kutokana na kukosa uzoefu (experience) na mtaji. Na sababu ya kufeli kwa yule aliyefaulu miaka mitano ya kwanza sio kutokana na mtaji bali ni kutokana na kuishiwa nguvu. Masaa mengi na juhudi kubwa wanazotumia katika majukumu yao kila siku ndani ya muda mrefu huwachosha na kufikia hatua mwili kuhitaji kupumzika....na hapo ndipo utakapokuta mtu anakosa juhudi kama zile alizokuwa nazo miaka iliyopita. Mfano kwa muuza duka, huchoka tena kuamka saa 12 kufungua duka kila siku na kwenda kulala saa 4 usiku au zaidi kama alivyokuwa anafanyaga zamani.... Na wanaofanikiwa kubaki hata ndani ya hiyo miaka kumi basi ni wale ambao wameendana na ile adha ya kuamka kila siku asubuhi, kwenda kazini na kufanya kazi kwa bidii maisha yao yote. Na mara nyingi inaonekana hiko ndicho pekee wanachokifahamu maishani na ambacho wameamua kukifanya. TUANZISHE BIASHARA ILA SIO ZA MTINDO HUU....TUTAFELI....YATUPASA TUANGALIE MBALI ZAIDI

No comments:
Post a Comment