Asilimia nyingi tu ya wananchi wa Tanzania ni maskini wa kiwango cha kutokuwa na kiasi chochote kile cha kuwekeza. Wenyewe tunasema tupo katika kiwango cha kuishi kusogeza siku mbele tu.
Ila cha kushangaza ni kwamba kuna baadhi ya wale wanaotengeza pesa nyingi wanaingia katika daraja hili. Hawa wanazalisha kiasi kingi ila pia wanatumia zaidi ya wanavyozalisha. Kuna muda mtu anaweza kuonekana TAJIRI sana. Ana mke mzuri, watoto watatu na wote wakawa wanasoma shule za kulipia (private schools). Yeye na mkewe wakawa wanaendesha magari ya kifahari. Na huenda akawa anakaa na familia yake katika jumba zuri kabisa na watoto wakikua wanaendesha magari ya kifahari pia. Machoni mwa watu wengi mtu kama huyu anaonekana ni TAJIRI sana lakini kumbe kiuhalisia huenda wakawa na madeni makubwa na ni maskini kuliko wale tunaowaona sisi ni maskini. Ukweli mchungu ni kwamba wengi wao kama sio wachache sio wawekezaji kwa maana hawana wanachokiwekeza.
(Naomba nisieleweke vibaya hapa---tukirejea maana ya WAWEKEZAJI ni wale wanaozalisha pesa zao kupitia vyanzo mbalimbali walivyowekeza bila ushiriki wao au ushiriki wao mdogo na sio wale wanazalisha pesa nyingi kupitia mishahara n.k). Baadhi kati ya wengi wanaomiliki magari...wananunua kupitia mishahara yao na si kutokana na UWEKEZAJI wao. Yaani siku mshahara ukikata tu tutaanza kutafutana. TUWEKEZE
Pia tuchukulie mfano wa msanii wa muziki yeyote yule ambaye anafanya vizuri kwenye muziki...wengi kama sio wote huwa wanaendesha magari na kuishi katika majumba ya kifahari n.k....Umegundua huwa inakuaje pale ambapo jina lake linapotea kwa muda au linapopotea daima....wengi wao wanaangukia katika dimbwi la umaskini kwa kuwa hawana vyanzo ambavyo wamewekeza na ambavyo vitazalisha bila hata ya uwepo wao....wengi wanategemea SHOW nyingi ndio ziwazalishie pesa na kusahau kuwekeza wanapozipata pesa hizo.
Tunachokipongeza kwa sasa wasanii wa kwetu hapa Tanzania wameamka.... @jumajux @mwanafa @vanessamdee @diamondplatnumz @officialalikiba wote hawa wamewekeza na tunazifahamu bidhaa zao....bila kuwasahau na wengine wengi ambao wamewekeza kwa ajili ya maisha ya baadae. HONGERA KWAO...Wakiendelea kuwekeza wataishi maisha ya kifahari milele.

No comments:
Post a Comment