elimuyautajiiri.blogspot.com

Wednesday, April 24, 2019

SOMO LA THELATHINI NA SABA



Leo tuongee kidogo kuhusiana na UHURU WA KUCHAGUA. Hakuna uhuru mkubwa zaidi ya kuishi utakavyo. Mara nyingi tumezoea wazazi wakijaribu kila namna ili watoto wao waishi namna ambavyo wanataka hususani katika masuala ya AJIRA yaani wazazi wengi wanatamani watoto wao wawe madaktari, mainjinia, wanajeshi nk 

Mwanzoni watoto hujitahidi kufanya kama wazazi wanavyotaka ila Kuna wakati unafika mtu anaamua kuishi yeye anavyohitaji sio tena kama ambavyo vile wazazi wao walivyoishi au walivyohitaji yeye aishi. Huenda familia yake iliishi kwa kutegemea mshahara ila yeye akaamua kutoishi ivo labda kwa kuwa aliona wazazi wake wakihangaika kila mwezi kuhakikisha mshahara wa mwezi huu unakutana na mshahara wa mwezi ujao. Hili huenda sio suala la kuwaumiza kichwa watu wengi, huenda wakawa wameyachagua maisha  hayo na kuyapenda tusigombane mana huo ndio UHURU WA KUCHAGUA ingawa kujaribu kuelimishana ni muhimu ila tunapaswa kuheshimu CHAGUO LA MTU ni maisha yake na yuko huru kuchagua.

Kuna watu wanapenda kuishi katika mfumo ambao mshahara wake kila mwaka unapanda daraja au anapanda cheo ila kuna watu hawataki kupitia njia hiyo. Kuna watu wanataka kuwa na ujuzi wa kipekee zaidi akijiajiri katika fani fulani, kuna wengine hawataki kusikia na hawajayachagua maisha hayo. Haishauriwi wote tufate njia kama aliyepita fulani HAPANA. Chagua njia unayoitaka na kuipenda halafu pita hiyo. Narudia tena ni CHAGUO LAKO , ISHI UNAVYOTAKA 

Kuna wengine wamesoma mpaka chuo kikuu na wakafika hatua wakaona kuwa kuendelea kutafuta shahada zingine sio jambo ambalo wao wamelichagua. Huenda wameona kuwa shule haifanyi watu kuwa matajiri maana ana ushahidi wa watu wengi waliosoma sana na sio MATAJIRI na yeye amechagua kuwa TAJIRI. 
Chagua njia unayoipenda na unahisi itakuletea furaha halafu pita. #IshiUtakavyoUsivunjeSheriaZaNchi#TusimsahauMungu
#SisiTumechaguaKuwaMATAJIRI

SOMO LA THELATHINI NA SITA


MATAJIRI WA KWELI ni wakarimu. Siku za usoni mungu akikujaalia ukawa TAJIRI basi usisahau kauli mbiu yao ya kutoa zaidi ndio kupata zaidi. Ukiwa TAJIRI unachotakiwa kufanya ni kuendelea kujifunza na kutoa kwa wengine. MUNGU atujalie tuwe MATAJIRI WA KWELI SIKU MOJA.
#MwekezajiDarajaLa5
#ItatuhusuSikuMoja
Kaa Tayari kwa somo Jipya
Attachments area

SOMO LA THELATHINI NA TANO


Kama hutaki kumkabidhi mtu pesa yako akuwekezee basi utakuwa unataka kupata elimu na kuweza kuzisimamia pesa zako wewe mwenyewe. Ukiona ivo jua unafaa kuwa mwekezaji namba 4 kuliko yule namba 3 anayemkabidhi mtu mwingine majukumu ya uwekezaji.... Na Kama unatufatilia hapa ukiwa  mwekezaji aliyebobea katika jambo fulani mf. masuala ya fenicha, makapeti, elimu n.k basi HONGERA SANA. Ni watu wachache sana wanaoamua kuwekeza muda wao katika kujifunza na kuweza kuzisimamia pesa zao.
Ili uweze kufanikiwa kama mwekezaji namba 4 (wawekezaji waliobobea katika jambo fulani n.k) ni kuendelea kujifunza, kuwa na walimu wazuri (watu waliokutangulia katika jambo hilo wakafanikiwa) bila kusahau marafiki ambao mnaendana fikra.
Wawekezaji namba 4  wanayaendesha maisha yao wakijua kwamba makosa yao ni nafasi kwao kujifunza na kukua zaidi na si vinginevyo. Hofu ya kuwekeza haiwatishi zaidi ya kuwapa MOTISHA.
Usisahau kutembelea 

elimuyautajiri. blogspot.com

SOMO LA THELATHINI NA NNE


Kama wewe ni mtunzaji wa pesa mzoefu (msevuji) kuwa makini sana hasa kama wewe unatunza pesa benki, kwenye kibubu au katika ule mpango wa kusubiria uipate pesa yako utakapostaafu. 

Kutunza pesa ni njia ya watu ambao hawataki kujifunza chochote kwani haihitaji maarifa yoyote ya pesa ili uweze kutunza pesa zako. Inasemekana unaweza mfundisha nyani kutunza pesa na akawa anatunza. Ubaya wa kutunza pesa ni kwamba unachojifunza ni kidogo sana na endapo pesa yako itateketea kwa namna yoyote ile utajikuta hauna pesa pia hakuna ulichojifunza chochote.

Kama wewe ni mtunzaji mzuri sana wa pesa basi unashauriwa kutafuta kozi zozote (elimu yoyote ya jambo fulani) zinazohusiana na uwekezaji na kuangalia kitu gani kitakuvutia halafu ukifanye. Kama hakuna kinachokuvutia kuwekeza basi endelea kutunza pesa zako.
Kuna msemo wa kizungu unasema "In General, SAVERS ARE LOSERS" naomba mnisaidie tafsiri hapa chini.... Usisahau kutembelea 


Attachments area

SOMO LA THELATHINI NA TATU


Kwa wale waliojitathmini  na kujiona kuwa wapo daraja la kwanza.
Kama hauna kitu chochote kinachokuingizia pesa na una vitu vingi vinavyokutolea pesa mfukoni basi wewe unaanzia katika daraja la chini kabisa yaani unaanza SIFURI. Na kama una madeni mengi basi uwekezaji wako mkubwa utakuwa ni kuondokana na hayo madeni. Hakuna ubaya kwa mtu kuwa na madeni labda kama haufanyi jitihada zozote. Unaweza kupoteza biashara na kuwa katika madeni makubwa na ikakuchukua muda kuondokana na madeni hayo mpaka kufikia sifuri yaani haudaiwi na mtu.
Kitu unachotakiwa kufahamu ni kwamba unatakiwa ujifunze kutokana na makosa na ukubali kukabiliana na lolote litakalotokea kutokana na makosa yako utakayoyafanya au uliyoyafanya na HILI NI FUNZO KUBWA UNALOTAKIWA KUFAHAMU KATIKA MAISHA YAKO YA KILA SIKU. Usipojifunza kutokana na makosa yako kamwe hautakuwa pale unapotaka kuwa siku moja.
Tutapeana mwongozo siku za usoni namna ambayo itakusaidia kuondokana na MADENI.
Usisahau kutembelea
elimuyautajiri.blogspot.com
Attachments area

SOMO LA THELATHINI NA MBILI


Kila mtu anaingia daraja moja au zaidi kati ya madaraja matano ya uwekezaji.....Wewe unahisi upo daraja gani? hebu jitathmini kwanza leo kabla ya somo lijalo.... Unataka kutoka kwenye hilo daraja na kwenda daraja lingine unalohisi ni zuri zaidi? Basi endelea kuwa hapa... Tunakuletea maarifa yatakayokuongoza kutoka kwenye hilo daraja usilolitaka...TURN ON POST NOTIFICATIONS...Uwe wa kwanza kupata maarifa hayo.

#MjulisheNaMwingine

Usisahau pia kutembelea


Attachments area

Friday, April 5, 2019

SOMO LA THELATHINI NA MOJA



(1) Mwekezaji daraja la 4 anatumia pesa yake kuwekeza ila Mwekezaji namba 5 anatumia pesa za watu wengine kuwekeza (kwa kuwa namba 5 anamiliki Biashara kubwa faida anayoipata ndio anayoitumia kuwekeza)

Na hii ndio tofauti kubwa kati ya wawekezaji hawa wawili. (2) Mwekezaji namba 4 anawekeza huku akiamini yeye ndio bora zaidi,
Mwekezaji namba 5 anawekeza huku akiamini katika ushirikiano wa wengine. Hii ikimaanisha kuwa sio lazima yeye ndiyo awe bora zaidi kuliko wengine bali timu yake kwa ujumla ndiyo iwe bora zaidi. Wengi wetu tunaamini kuwa kuwa vichwa viwili ni bora kuliko kichwa kimoja lakini wengi pia bado tunaendelea kuamini kuwa sisi ni bora kuliko watu wote. (kama bado unajiona hivi jua wewe ni MWEKEZAJI DARAJA LA NNE) (3) Mwekezaji namba 4 anazalisha pesa chache ukilinganisha na mwekezaji nambari 5. (4) Mwekezaji namba 4 pia anasimama kama mtu MBINAFSI na jinsi anavyozidi kuwa mbinafsi ndio jinsi anavyotengeneza pesa zaidi. Tuchukulie mfano wa MC mzuri wa sherehe …unajua ili atengeneze pesa nyingi iweje? Inabidi apate madili mengi zaidi, sasa chukulia kapata madili 10…akimstua mwingine afanye walau mawili kati ya hayo kumi si pesa kwake inapungua??? Kama sio UBINAFSI ni nini huo?
Mwekezaji namba 5 anasimama kama mtu MKARIMU, jinsi anavyokuwa mkarimu ndio jinsi pesa inavyoingia zaidi. Mtu kukupa kazi tutauchukulia kama UKARIMU sio? Tunamsemeaje mtu anayefanya biashara ya duka na kila linapokua anafungua sehemu nyingine na kumuweka mtu….Hii haimaanshi kila anapokuwa MKARIMU zaidi basi na pesa inaingia zaidi??? (5) Ni ngumu kukuza mtaji ukiwa na MTAZAMO KAMA WA MWEKEZAJI DARAJA LA NNE (mf. Lazima niwepo mimi mwenyewe ili biashara iende vizuri, akikaa mwngine mambo hayaendi vizuri). Na ni rahisi sana kukuza mtaji ukiwa na mtazamo wa mwekezaji namba TANO (mf. Hili duka langu likikua nitafungua lingine sehemu fulani halafu nitamuweka fulani sio lazima niwe mimi ili biashara iende vizuri). Mtu akifahamu tu namna ya kuifanya biashara yake ikawa kubwa basi mafanikio hayo yataleta pesa nyingi zaidi. Inakuwa rahisi sana kutengeneza pesa kupitia UWEKEZAJI kama utafanikiwa kuikuza biashara yako ikawa kubwa.

Usisahau kutembelea 


SOMO LA THELATHINI



Hakuna maelezo mengi sana juu ya hawa watu zaidi ya kusema kuwa daraja hili ni la wamiliki wa biashara walioamua kuwekeza na ni daraja ambalo wote tunaotaka kuwa MATAJIRI wa kweli yatupasa kulilenga. Tambua tu kuwa hapa ndipo ambapo MATAJIRI wengi wakubwa duniani wanapatikana. Maelezo yao mengi tunaweza yapata kupitia utofauti wao na daraja la nne. #TofautiPostIjayoMudaSiMrefu
Usisahau kutusapoti kwa kutembelea


SOMO LA ISHIRINI NA TISA



Hawa ni wale ambao wanahisi wanaweza kufanya kila kitu wenyewe, wengi ya waliostaafu huingia katika daraja hili pindi muda wao wa kufanya kazi unapoisha.  Mfano kama anataka kuwekeza katika jambo fulani kila kitu atafanya yeye mwenyewe kama kufanya utafiti wa eneo zuri la kufanya uwekezaji wake, kutafuta wateja, kufanya marekebisho yoyote, gharama zozote zile ataingia kwa pesa zake n.k
Mara nyingi watu ambao wanahisi wanaweza kufanya kila kitu wenyewe wanakuwaga na elimu ndogo  kuhusiana na mambo ya pesa. Na hata wakipata nafasi ya kupata elimu basi wanaegemea katika eneo husika wanalolipenda kupitia kozi moja au mbili.
Jua kwamba hili daraja sio tu kwa wastaafu bali ni daraja ambalo watu wengi tunaopata mawazo ya kuwekeza tunaangukia..... yaani wengi tunawekeza lakini katika uwekezaji wetu wengi tunaona kila kitu tunaweza kufanya wenyewe au mpaka tuwepo wenyewe ndipo mambo yatakapoenda vizuri zaidi.
Huku wengine wakisema kuwa hakuna anayeweza kufanya vizuri zaidi ya wanavyofanya wao yaani tunajiona ni wa kipekee zaidi katika eneo letu fulani tulilobobea tukisahau kwamba kuwaza hivyo kunatuchelewesha kuwa MATAJIRI wa kweli.

Usisahau kutusapoti kwa kutembelea 

Face the challenge